Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuondolewa kwa Rais wa Niger madarakani kwazua hofu

Mohamed Bazoum Kuondolewa kwa Rais wa Niger madarakani kwazua hofu

Sat, 21 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya sintofahamu inayomkabili Rais aliyeondolewa madarakani nchini Niger, Mohamed Bazoum, imezua wasiwasi ambapo Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anataka awe huru.

DW imeripoti kuwa Macron ametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa kiongozi huyo pamoja na familia yake.

Tangu kupinduliwa na jeshi la nchi hiyo Julai 26, mwaka huu, Bazoum amekuwa akizuiliwa katika makazi yake pamoja na familia yake.

Mawakili wa Bazoum wamepinga kushikiliwa kwake wakisema kuwa utawala wa kijeshi umekiuka haki za msingi kwa kumshikilia Rais huyo sehemu isiyojulikana.

Hali hii inaendelea kuzua wasiwasi huku viongozi wa kijeshi wakisema wamezuia jaribio la kiongozi huyo kutaka kutoroka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live