Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kundi la kigaidi latangaza kuhusika mauaji ya wanajeshi Burkina Faso

Mashambulizi 50 Burknafaso.jpeg Kundi la kigaidi latangaza kuhusika mauaji ya wanajeshi Burkina Faso

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa, limehusika kwenye mauaji ya zaidi ya wanajeshi 70 na kujeruhi wengine kadhaa na kutekwa nyara watu watano wakati wa shambulizi la kushtukiza dhidi ya msafara wa kijeshi kaskazini mwa Burkina Faso.

Taarifa zaidi zinasema, kundi hilo liliushambulia msafara uliokuwa unajaribu kusonga mbele kwenda kwenye maeneo wanayoyadhibiti karibu wa Deou katika jimbo la Oudalan huko Sahel.

Ripoti zimeongeza kuwa, wanajeshi hao walipokonywa silaha, pamoja na kufukuzwa kwa maili kadhaa ndani ya jangwa. Picha zilizotolewa na kundi hilo zimeonyesha miili 54 ya wanajeshi waliovalia sare, zaidi ya bunduki 50 walizopora, pamoja na wanajeshi watano waliotekwa nyara.

Shambulizi hilo limefanyika wiki moja baada ya jingine kwenye eneo hilo na siku kadhaa baada ya lile ambalo lilifanyika kwenye mji wa Tin Akoff ambako wakazi na mashirika ya kiraia wanasema kwamba, dazeni ya wanajeshi pamoja na raia waliuwawa, baada ya shambulizi dhidi ya kituo kimoja cha kijeshi.

Hayo yanajiri siku chache tu baada ya magaidi wasipoungua 160 kuangamizwa katika operesheni ya jeshi la Burkina Faso katika eneo la Sahel.

Maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni mbili wamekimbia makazi yao tangu magaidi hao wakufurishaji waanze kuishambulia Burkina Faso kutokea nchi jirani ya Mali mnamo 2015.

Hujuma na mashambulio ndani ya ardhi ya Burkina Faso yamechochea kuzuka mapinduzi mawili mwaka jana yaliyofanywa na maafisa wa jeshi waliokasirishwa na kuongezeka idadi ya raia wanaouawa katika mashambulio hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live