Juhudi za kujenga upya, sehemu ya jukwaa liliporomoka katika uwanja wa michezo wa Martyrs ambako Papa Francis atakuwa na misa kubwa siku ya Alhamisi (Februari 2, 2023), nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC zinaendelea.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo, imeeleza kuwa sehemu ya jukwaa hilo lililopo ndani ya uwanja huo wa michezo jijini Kinshasa, iliporomoka kwa sababu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis anatarajiwa kuwasili nchini DRC hii leo Januari 31, 2022, kuanza ziara ya kihistoria na siku ya Ijumaa anatarajia kwenda nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kuendeleza ziara yake.
Hata hivyo, maandalizi rasmi ya kumkaribisha Papa Francis yamekamilika, na wakongo wengi wana shauku ya kusikia kile ambacho kitasemwa kupitia hotuba yake kwa Taifa hilo lililokubwa na ghasia na machafuko.