Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Kuna hofu na wasiwasi mwingi' wanahofia kuwa M23 wanaweza 'kuuteka' mji

'Kuna Hofu Na Wasiwasi Mwingi' Wanahofia Kuwa M23 Wanaweza 'kuuteka' Mji 'Kuna hofu na wasiwasi mwingi' wanahofia kuwa M23 wanaweza 'kuuteka' mji

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Baadhi ya wakazi wa Goma, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, wanasema wanahofia kwamba waasi wa M23 sasa wanalenga kuuzingira mji huo na kuufanya usiweze kufukiwa.

Hii ni baada ya M23 kusema kuwa inadhibiti kituo cha Shasha kwenye barabara kuu ya Goma-Sake-Minova-Bukavu.

Kwa kawaida, Goma – mji uliopo kando ya Ziwa Kivu, hupata zaidi ya 90% ya chake hutoka maeneo ya jirani ya Rutshuru na Masisi, ambayo yanayopatakana na barabara kuu nne zifuatazo:

Goma – Rutshuru – Butembo (pia kwenda/kutoka mpaka wa Bunagana) Goma – Sake – Masisi Kati (Masisi Centre) Goma – Sake – Kitchanga

Kundi la M23 linasema linadhibiti maeneo ya karibu na Sake, na Norbert Nangaa, mkuu wa kundi la AFC na M23, alionekana kwenye video akisema kuwa siku ya Ijumaa "majeshi yangu yaliiteka Shasha, na kuizingira Sake".

Barabara tatu za kwanza sasa zinapita katika maeneo yanayodhibitiwa na M23, na kwa sasa sasa sio njia zinazofaa kutumiwa na raia kwenda au kutoka Goma.

Juhudi za BBC za kuzungumza na vikosi vya serikali hazikufua dafu, na hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka upande huo kuhusu mapigano makali ambayo yamedumu kwa siku kadhaa na kuendelea mwishoni mwa juma.

Baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza Jumatatu kuwa vikosi vya serikali vitarejea katikati ya Shasha, jambo ambalo bado halijathibitishwa na upande wa serikali.

Chanzo: Bbc