Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kufutwa makubaliano ya kijeshi kati ya Niger na Umoja wa Ulaya

Niger Na Umoja Wa Ulaya Kufutwa makubaliano ya kijeshi kati ya Niger na Umoja wa Ulaya

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya kijeshi ya Niger ilitangaza Jumatatu kuwa imefutilia mbali makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuimarisha jeshi la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, viongozi wa Niger walitangaza Jumatatu kumalizika shughuli za wajumbe wawili wa ulinzi na usalama wa Umoja wa Ulaya nchini humo baada ya kukubaliana na Russia juu ya kuimarisha ushirikiano wa kijjeshi wa pande mbili.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Niger imeeleza kuwa mmoja wa wajumbe hao anaendesha shughuli zake katika mji wa Niamey chini ya mkataba, wa "UCAP Niger Coast", ambayo ni matokeo ya makubaliano ya zamani na Umoja wa Ulaya ya kuimarisha uwezo wa jeshi la nchi hiyo.

Taasisi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2012, ilikuwa inatoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya ndani, mamlaka na vituo vya binafasi vya Niger.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Niger imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba serikali imesimamisha shughuli zake zote na Ujumbe wa Ushirikiano wa Kijeshi wa Umoja wa Ulaya.

Niger imekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum, kuondolewa madarakani na jeshi mwezi Julai.

Viongozi wa kijeshi wa Niger baada ya kumuondoa madarakani Bazoum, ambaye alikuwa mwitifaki wa Ufaransa, walitaka kuondolewa nchini humo wanajeshi wa Ufaransana na baada ya uamuzi huo Paris imeanza kuwaondoa wanajeshi wake 1,500 katika nchi hiyo.

Siku ya Jumatatu, ujumbe kutoka Russia ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo ulifanya mazungumzo na viongozi wa Niger mjini Niamey ambapo nchi hizo zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao wa kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live