Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuanzia leo saa 9 Alasiri, raia wa nchi 6 za Afrika hawaruhusiwi kuingia Uingereza

Asdfdg Kuanzia leo saa 9 Alasiri, raia wa nchi 6 za Afrika hawaruhusiwi kuingia Uingereza

Fri, 26 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasafiri wanaowasili nchini Uingereza kutoka mataifa tofauti ya Afrika watalazimika kujitenga huku kukiwa na onyo kuhusu aina mpya ya virusi vya corona.

Waziri wa afya nchini Uingereza Sajid Javid alisema siku ya Ijumaa kwamba mataifa sita yataongezwa katika orodha , huku baadhi ya ndege zikipigwa marufuku kwa muda.

Mtaalamu mmoja alitaja virusi hivyo vipya kwa jina B1.1.529, kuwa hatari zaidi kuonekana kufikia sasa na kuna wasiwasi kwamba vina uwezo wa kukwepa kinga.

Hakuna hata kisa kimoja cha virusi hivyo kimeripotiwa nchini Uingereza. Ni wagonjwa 59 pekee waliogunduliwa nchini Afrika Kusini , Hong Kong na Botswana kufikia sasa.

Ndege zilizopigwa marufuku ni Afrika Kusini , Namibia, Lesotho, Eswatini, Zimbabwe na Botswana na raia wake hawatoruhusiwa kuingia nchini humo kwa muda.

Bwana Javid alisema kwamba wanasayansi walikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu virusi hivyo vipya lakini mengi yanahitajika ili watu kujifunza kuvihusu.

Je tunajua nini kuhusu aina mpya ya kirusi cha Corona cha B.1.1.529 Lakini alisema kwamba virusi hivyo vipya vinabadilika mara kadhaa , pengine maradufu ya jinsi virusi vya Delta vinavyojibadilisha.

Aliongezea: Na hilo lina maana kwamba huenda vinaweza kusambaa kwa urahisi na kwamba chanjo tulio nayo kwasasa huenda ni hafifu.

Aliongezea kwamba kuyaongeza mataifa hayo sita katika orodha ya mataifa yaliopigwa marufuku kwa muda ilikuwa hali ya kuchukua tahadhari na hatua ili kujaribu kulinda kwa njia yoyote, mipaka yetu.

Kuanzia saa tisa mchana siku ya Ijumaa raia wasio wa Uingereza pamoja na wale wa kutoka Ireland watapigwa marufuku kuingia England iwapo watakuwa wametoka katika nchi sita katika kipindi cha siku 10 zilizopita.

Raia yeyote wa Ireland au Uingereza anayewasili kutoka mataifa hayo baada ya saa moja siku ya Jumapili atalazimika kujitenga katika hoteli , huku wale wanaorudi kabla ya siku hiyo wakitakiwa kujitenga nyumbani.

Wale ambao wamerudi katika kipindi cha siku 10 wanatakiwa kufanyiwa vipimo vya corona na idara ya afya Uingereza UKHSA

Marufuku hiyo ya safari za ndege itasalia hadi mfumo wa kujitenga katika hoteli utakaposhika kasi.

Marufuku hiyo ya safari za ndege itasalia hadi mfumo wa kujitenga katika hoteli hiyo utakaposhika kasi.

Uchambuzi wa James Gallagher,- Mwandishi wa Afya na sayansi Mwanasanyansi mmoja aliniambia aina hii ya virusi ndio hatari zaidi kuwahi kuiona - unapoitazama sio vigumu kuiona kwanini.

Ndio inayojibadilisha wakati mwingi zaidi kufikia sasa na ni tofauti na ile iliopatikana Wuhan , China.

Hiyo ina maana kwamba , chanjo zilizotengenezwa kwa kutumia kirusi cha kwanza hazina uwezo .

Na baadhi ya mabadiliko yake yanadaiwa kuongeza uwezo wa virusi vya corona kusambaa.

Lakini kumekuwa na aina chungu nzima ambazo ni hatari zaidi lakini hazijaanza kusambaa.

Kuna ishara za mapema kwamba virusi hivi vinasambaa Afrika kusini na kwamba huenda vipo katika kila mkoa wa taifa hilo.

Lakini swali kuu -je aina hiyo inaweza kukwepa chanjo mara ngapi, je ni hatari, je inasambaa kwa haraka zaidi ya virusi vya Delta- maswali hayo hayana majibu kwa sasa.

Mwandishi wa BBC Andrew Harding anasema kwamba wanasayansi nchini Afrika kusini walikuwa wakijaribu kuelewa mabadiliko ya hiyo aina mpya ya virusi lakini kitu kimoja ambacho hawakujua ni kwamba kilikuwa kinaambukizwa kwa urahisi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live