Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa Kutafuna Pesa Alizotumiwa Kimakosa M-Pesa

Mahakama22 Mtuhumiwa Mahakamani

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMAMA Nancy Chonge Chepkwemoi nchini Kenya ameshtakiwa kwa tuhuma za kuiba pesa alizotumiwa kimakosa kupitia simu kutoka kwa Vincent Maina Wambutu mnamo Novemba 27 kinyume na kifungu cha 268 (1) cha kanuni ya adhabu.

Imeelezwa kuwa Wambutu alikuwa akituma pesa kutoka kwenye akaunti yake ya benki kwenda akaunti ya M-Pesa lakini akaingiza nambari isiyo sahihi na kutuma pesa hizo kwa Chepkwemoi kimakosa.

Hakujua hadi siku iliyofuata alipojaribu kumtafuta Chepkwemoi kwa njia ya simu yake, ilikuwa imezimwa, alimtumia ujumbe mfupi kisha aliripoti kisa hicho kwa benki akiomba kurejeshewa pesa hizo lakini baadaye akaambiwa itakuwa vigumu kwani tayari hela hizo zilikuwa zimeshatolewa.

Chepkwemoi aliwasha simu yake baada ya siku tatu lakini hakuwasiliana na Wambutu wala kumrejeshea pesa. Wambutu aliripoti kisa hicho katika kituo cha polisi cha Parklands na Chepwkemoi alifuatiliwa na kukamatwa kisha kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Renee Kitangwa wa Mahakama ya Kibera alikana kuhusika na mashtaka hayo ambapo aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu KSh 50,000 na kesi hiyo itatajwa tena Desemba 21, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live