Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Korona iko wenzangu, Rais wa Tanzania Samia Suluhu awaambia raia wake

44339f889f5a8e5f Korona iko wenzangu, Rais wa Tanzania Samia Suluhu awaambia raia wake

Mon, 28 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magufuli aliishi kuwarai wananchi kuamini kuwa maombi yalikuwa yameshida vita dhidi ya coronavirusRais Suluhu Jumamosi Juni 26 alichukua mkondo mpya na kukiri kuwa kuna maambukizi ya maradhi hayo nchini humoAliwataka wananchi kuanza kuvalia maski kama njia moja ya kukabiliana na maradhi hayo yanayotikisa duniaRais wa Tanzania Samia Suluhu amechukua mkondo tofauti wa uongozi na aliyekuwa mtangulizi wake John Pombe Magufuli.

Tofauti na Magufuli, Suluhu amekiri kuwa maradhi ya coronavirus yamo nchini humo na kuwataka raia kuchukua tahadhari.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Twitter, Samia aliwataka raia kuanza kuvalia maski ili kujikinga maambukizi.

"Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona (Uviko-19) kama tunavyoelekezwa na wataalamu wetu wa afya," alisema Suluhu.

Kwa amra ya kwanza, huenda raia wa nchi hiyo wakaanza kuvalia maski kama vile imekuwa sehemu zingine duniani.

"Tunawe mikono kwa maji tiririka na sabuni, tutumie vitakasa mikono, tuvae barakoa na tusigusanegusane. Ugonjwa wa Korona upo" aliongeza Rais Samia.

Wakati wa uongozi wa Magufuli, alipiga marufu uvaliaji wa maski nchini humo akisema walikuwa wameshinda vita dhidi ya coronavirus.



Mwezi Juni 2020, Magufuli alikuwa amewashukuru washirika wa kanisa akisema wamekuwa wakiomba Mungu kumaliza Covid-19.

"Nataka niwashukuru Watanzania kutoka dhehebu zote. Tumekuwa tukiomba Mungu atuokoe kutokana na janga hili na amejibu maombi yetu. Ninaamini na ninajua Watanzania wengi wanaamini kuwa ugonjwa huo umemalizwa na Mungu," alisema

Rais SUluhu hata hivyo baada ya kuchukua mamlaka aliahidi kuwa wataalamu watafanya uchunguzi wao ili kushauri serikali kuhusu maradhi hayo kuwa nchini humo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke