Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongo yaanzisha mazungumzo na Zambia kufungua mpaka

Zambia DRC Kongo yaanzisha mazungumzo na Zambia kufungua mpaka

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kongo imeanza mazungumzo na Zambia siku chache baada ya taifa hilo jirani upande wa kusini kutangaza kuufunga mpaka wake na Kongo ambao ni lango muhimu la usafirishaji bidhaa baina ya nchi hizo mbili.

Mnamo siku ya Jumamosi, Waziri wa Biashara wa Zambia Chipoka Mulenga alitangaza kuufunga kwa muda mpaka huo baada ya kuzuka maandamano kwenye mji wa mpakani wa Kasumbalesa. Maandamano hayo yalifanywa na wasafirishaji bidhaa waliokuwa wakipinga uamuzi wa Kongo wa kuzuia kuingizwa vinywaji na vileo kutoka Zambia.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya biashara ya Kongo, imesema mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na Zambia yanafanyika ili kuwezesha kufunguliwa kwa eneo hilo la mpaka haraka iwezekanavyo.

Wawakilishi wanapanga kukutana mjini Lubumbashi kutafuta suluhisho la kudumu juu ya mahusiano ya kibiashara kati nchi ya nchi hizo jirani.

Kongo iliyo mzalishaji mkubwa wa pili duniani wa madini ya shaba inatumia njia za mataifa jirani ikiwemo Zambia kusafirisha malighafi hiyo kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live