Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kongano la 16 la SWIRMO lafanyika Kenya

Kenya Kongamano.png Kongano la 16 la SWIRMO lafanyika Kenya

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati huu dunia inapondelea kushuhudia mizozo katika mataifa mbalimbali, viongozi wa kijeshi wamekongamana jijini Nairobi, Kenya kujadili ni vipi sheria za kimataifa za kulinda haki za binadamu zitazingatiwa wakati wa mizozo.

Katika ufunguzi wa kongamano hilo la juma moja , waziri wa ulinzi wa Kenya Aden Duale, amesema mkutano huu umefanyika kipindi hiki dunia ikishuhudia vita kati nchi mbalimbali akiriri haja ya sheria za kimataifa kutumika kuzia machafuko zaidi.

Waziri Daule aliongoza kuwa Hali ya sasa ya dunia, inakumbusha kila afisa wa jeshi haja kuzingatia sheria za kimataifa za kulinda haki, ili kuzuia misongamano ya majanga, inayotokana na vita, na kuongeza kuwa serikali ya Kenya itandelea Kushirikiana na Kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC kulinda maisha.

Kwa upande wake naibu mkuu wa jeshi nchini Kenya, Leteni kanali John Mwangi, ambaye alimwakilisha mkuu wa majeshi nchini Kenya, Francis Ogolla kwenye hafla hiyo, amesisitiza haja ya wanajeshi kote duniani kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa katika maeneo ya vita na kuzuia maafa ya raia wasiokuwa na hatia.

Luteni kanali John Mwangi, nasema kazi ya wanajeshi katika uwanja wa mapambano ni kuzuia maafa na kutofautisha kati ya wahalifu na wale ambao si wahalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live