Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kombora nchini Sudan lasababisha vifo vya takriban watu 22

Kombora Nchini Sudan Lasababisha Vifo Vya Takriban Watu 22 Kombora nchini Sudan lasababisha vifo vya takriban watu 22

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Kombora la jeshi la Sudan lawaua watu 22 na kuwajeruhi wengine wengi mashahidi na afisa wa serikali wanasema.

Wanawake na watoto ni miongoni mwa waathiriwa, mashahidi hao wameiambia BBC.

Kombora hilo lilianguka wilayani Omdurman, katika upande wa pili wa ufukwe wa mto Nile kuelekea mji mkuu Khartoum mapema Jumamosi.

Vikosi vya jeshi vimekuwa vikikabiliana kupata udhibiti wa mji mkuu tangu April.

Mzozo huo ulianza baada ya mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na mkuu wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, walipo tofautiana kuhusu mustakabali wan chi.

Afisa wa afya katika jimbo la Khartoum amenukuliwa na shirika la Habari Reuters akisema takriban watu 22 wamueawa katika kombora la Jumamosi, wakati RSF likisema idadi ya waliofariki ni watu 31.

Kikosi hicho cha jeshi kimeongeza katika taarifa yake kwamba kombora hilo la angani limesababisha " uharibifu mkubwa katika makaazi ya watu".

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema "ameshutushwa" na ghasia hizo na ana wasiwasi kwamba huenda mzozo huo ukaishia kuwa vita kamili vya ndani ya nchi, " ambavyo vina uwezo wa kuitikisa kanda nzima". Ametoa wito kwa pande zote mbikui kusitisha mapigano na kuwalinda raia.

Chanzo: Bbc