Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha mpya Gor aanza kwa ushindi

105693606146fc87833c4bb6e6f4758c Kocha mpya Gor aanza kwa ushindi

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA mpya wa Gor Mahia, Carlos Pinto amewataka wachezaji wake kuendelea kujituma baada ya kuanza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mathare United kwenye Uwanja wa Kasarani Annex.

Mreno huyo aliteuliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Roberto Oliveira na badala ya kuwafanyisha wachezaji mazoezi kwa siku tatu, aliisaidia klabu kurejea katika ushindi.

Pinto alisema wachezaji walikuwa wakifanya mazoezi kwa bidii na siku ya mechi aliwataka kufanya kweli.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa Gor Mahia dhidi ya vijana hao kutoka maeneo ya mabanda katika kipindi cha miaka minne.

"Nilikuwa na siku tatu tu za kuwaandaa wachezaji baada ya mechi ya wiki iliyopita dhidi ya Kariobangi Sharks. Tulishinda kwa sababu wachezaji walikuwa wakijituma katika mazoezi na kucheza kwa maelekezo.

Ushindi huo ni hatua chanya kuelekea ndoto zangu kurejea katika ligi na kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, alisema kocha huyo mwenye leseni ya Uefa.

Wakati huohuo, Pinto alibainisha kuwa safu ya ulinzi ndio eneo lake la kwanza kulishughulikia baada ya kuiona timu yake ikilala kwa mabao 4-3 dhidi ya Sharks mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Wakati wa mchezo wa Sharks nilibaini kuwa timu ina matatizo katika safu yake ya ulinzi, hasa kuzuia mipira ya adhabu, lakini nitawafunza vijana jinsi ya kuzuia na nina furaha vijana walicheza vizuri dhidi ya Mathare," aliongeza.

Chanzo: habarileo.co.tz