Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiwanda 'fake cha Iphone chanaswa Msumbiji

Iphone 14.jpeg Kiwanda 'fake cha Iphone chanaswa Msumbiji

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka zimegundua uwepo wa kiwanda haramu kinachotengeneza simu za Kampuni ya AppleInc bandia katika Mji Mkuu Maputo, ambapo walinasa simu 1,165.

Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Raia wawili wa China, kiliweza kutekeleza taratibu za kiufundi wa simu hizo, kama vile kuunganisha (assembly) na kugawa namba za IMEI, ambayo hurahisisha utambuzi wa uhalali wa kifaa.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Forodha, Gino Jone amesema kuna tuhuma kwamba baadhi ya simu za mkononi huenda zimeibiwa kwa sababu hakuna hati inayohalalisha uingizwaji na uuzwaji wao sokoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live