Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitu Ilikuwa Safi: Tume ya IEBC yapuuza madai ya wizi wa kura Kiambaa

2ba4119e9c4e8d92 Kitu Ilikuwa Safi: Tume ya IEBC yapuuza madai ya wizi wa kura Kiambaa

Sat, 24 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

IEBC imekanusha madai ya kuwepo njama za wizi wa kura katika uchaguzi mdogo wa KiambaaTume hiyo imekashifu baadhi ya wanasiasa ikisema wanaipaka tope na madai yasiyo ya kweliIlisema huenda hilo likahatarisha uchaguzi mkuu ujao wa 2022 iwapo mkondo huo utaendeleaTume huru ya mipaka na uchaguzi nchini IEBC imewataka wansiasa kukoma kuipaka tope kutokana na matokeo ya chaguzi ndogo za Kiambaa na Muguga.

IEBC ilisema ilitekeleza kazi yake kwa umakini na kuhakikisha kuwa matokeo yalikuwa ya uwazi na kwa mujibu wa mapenzi ya wapiga kura.

Kupitia kwa taarifa Alhamisi Julai 22, IEBC ilisema inachomwa roho na baadhi ya wansiasa ambao wamekuwa akisema kura ziliibwa.

"IEBC inahuzunika kuhusu matamshi yaliyotolewa na Seneta wa Kiambu Kimani wa Matangi ambaye alishuku uhalali wa matokeo yaliyotolewa wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiambaa" IEBC ilisema.



Kwa mujibu wa tume hiyo, iwapo kuna mgombea alipata kura sawia katika vituo tofauti itakua ni kutokana na sadfa tu na wala si njama yoyote.



Read also

Katibu wa COTU Francis Atwoli Asema Anashuku Ziara za DP Ruto Uganda

Tume hiyo ilisema ni makosa kwa wanasiasa kuipaka tope ikisema hilo litakuwa na athari mbaya zaidi wakati huu taifa linaelekea uchaguzi mkuu ujao.

"Mashambulizi yanayoelekezewa IEBC inaharibu jina lake na pia kuweka mkondo hatari wakati huu ambapo tunaelekea uchaguzi mkuu ujao," mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kwenye taarifa.

Wanasiasa wanaoegemea upande wa Jubilee amekuwa wakitilia shaka matokeo ya Kiambaa ambapo mgombea John Njuguna alimshinda Kariri Njama wa Jubilee.

Kariri alisema ataelekea mahakamani kupinga matokeo hayo huku akitaka kura kuhesabiwa upya katikavituo vya Kawaida na Mchatha.

Naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe alisema ana imani kuwa chama chake ndicho kilishinda uchaguzi huo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke