Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiti cha rais wa Ghana kinachobebwa na gari la kifahari chazua gumzo mitandaoni

Kiti Ghana Kiti cha rais wa Ghana kinachobebwa na gari la kifahari chazua gumzo mitandaoni

Thu, 13 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mitandao ya kijamiii nchini Ghana imekuwa na gumzo kuhusu mipango ya safari ya Rais Nana Akufo Addo. Kuna madai kuwa kiti cha kifahari cha ngozi ya rangi kahawia - kinachotumiwa na rais kwa matumizi yake binafsi kina gari lake la kukisafirisha popote anapokwenda.

Kulikuwa na ripoti kwamba gari la Toyota V8 ndilo ambalo hutumiwa kukisafirisha kiti hichoambacho kina dereva wake maalum na maafisa wa ulinzi

Waliotoa maoni yao kuhusu Habari hizo walisema ni jambo la kushangaza kuzitumia raslimaliza umma kwa njia hiyo .

Aliyekuwa rais wan chi hiyo John Mahama alisema yeye mwenyewe amewahi kushuhudia kiti hicho kikisafirishwa kwa njia hiyo wakati rais Nana alipokuwa akihudhuria mazishi ya jaji mmoja .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live