Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiswahili kuanza kutumika rasmi katika vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kiswahili Kiswahili Kiswahili Kiswahili kuanza kutumika rasmi katika vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC imetangaza rasmi kwamba kuanzia mwaka huu lugha ya Kiswahili itaanza kutumika rasmi katika vikao na mikutano yake yote pamoja na nyaraka zote kutolewa kwa lugha hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Peter Mathuki amenukuliwa na Shirika la Habari la Umoja wa Mataifa akisema kuwa tayari bajeti ya jumuiya ya 2023 imepitishwa na ina fungu la kuwezesha lugha tatu kutumika ambazo ni Kingereza, Kifaransa na Kiswahili.

Amesema, Kiswahili kinategemewa sana kwa sababu wananchi wengi katika jumuiya yetu wanaelewa lugha ya Kiswahili kwa hiyo ni jukumu la jumuiya kuhakikisha kwamba habari zote na vikao vyote vinafanyika kwa lugha ya Kiswahili.

Dkt. Mathuki aidha amebainisha sababu ambazo zimepelekea kuchukue muda mrefu kwa lugha hiyo kuanza kutumika kwa kubaini kuwa: “Shida ilikuwa ni Kiswahili hakikuwepo kwenye katiba ya jumuiya, lakini sasa baada ya kusema turekebishe katiba ya jumuiya na kuweka lugha hiyo si tu bungeni bali kwenye vikao vyote vya jumuiya na hiyo sasa tumeanza mikakati yake.” Dkt. Peter Mathuki

Mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika Novemba mwaka jana Arusha Tanzania na kuridhia nchi ya Somalia kujiunga rasmi na jumuiya hiyo kama mwanachama na kuwa mwanachama wa nane akijiunga na nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC.

Ikumbukwe kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetangaza tarehe 7 ya mwezi Julai kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

Aidha Muungano wa Afrika (African Union) mwaka 2022 ulipitisha lugha ya Kiswahili, kuwa lugha rasmi ya kikazi ndani ya Umoja huo. Lugha hiyo huzungumzwa katika nchi kadhaa za mashariki, kati na kusini mwa Afrika pamoja na jamii kubwa za Waswahili katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na Oman.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live