Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KirusiKipya: Maambukizi yazidi kupanda Afrika Kusini

Covid South Maambukizi yazidi kupanda Afrika Kusini

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kasi ya maambukizi ya kirusi kipya aina ya Omicron cha Corona nchini Afrika Kusini yazidi kupamba moto kila siku tangu kilipotangazzwa kuingia nchini humo.

Maambukizi hayo yameongezeka kutoka 26,485 ya mwezi Julai hadi 26,976 mwezi Septemba ambayo ilirekodiwa kufuatia wimbi la tatu lililosababishwa na kirusi cha Delta.

Kirusi hiki kipya cha Omicron ambacho kimegunduliwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwezi Novemba kimezua taharuki kubwa duniani kwa kile kinachodaiwa kuwa kinasambaa kwa kasi zaidi kuliko virusi vingine vilivyopita.

Hadi sasa nchi hiyo inaripoti jumla ya vifo 108 vya ugonjwa huo kwa siku, idadi ambayo inatajwa kuwa juu zaidi duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live