Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KirusiKipya: Maambukizi yazidi Kenya

Majestic Cell Corona E1584032867403 660x400.png #KirusiKipya: Maambukizi yazidi Kenya

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maambukizi ya Corona nchi kenya yanatajwa kuongezeka zaidi tangu taifa hilo lilipotangaza kwa mara ya kwanza uwepo wa kirusi hicho mwezi Machi 2020.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya zinaonesha ongezeko kubwa la wagonjwa ambao hadi sasa wanafika takribani asilimia 29.6, ongezeko ambalo limechangiwa na uwepo wa kirusi kipya cha Omicron.

Wataalam wa afya nchini humo, wameishauri Serikali kuzingatia na kuweka mashariti mapya yatakayopunguza kasi ya maambukizi ili kuepuka athari zinazoweka kujitokeza kama vile vifo.

Nalo Shirka la Afya Duniani, WHO limeitaja nchi hiyo kuwa miongoni mwa mataifa yaliyo kwenye hatari zaidi ya kuathirika na kirusi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live