Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KirusiKipya: Kenya yakataa kuweka lockdown tena

Kagwe Kenya yakataa kuweka lockdown tena

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Kenya imesema kuwa haitaweka marufuku ya kutotoka nje licha ya kutangazwa kwa kirusi kipya aina ya Omicron cha Corona kilicholetwa na wasafiri wawili wa Kenya na Mwafrika Kusini mmoja aliyeingia nchini humo wiki iliyopita.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema Kenya badala yake imejikita katika kutoa chanjo kwa raia wake ikiwa ni juhudi za kuzuia kuenea kwa kirusi hicho.

"Hatutatangaza marufuku ya kutotoka nje hivi karibuni. Njia pekee ya kuzuia hili ni chanjo, "amesema Kagwe.

Hata hivyo tangazo hilo limekuja saa chache baada ya kusema hakuna visa vipya nchini humo licha ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live