Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#KirusiKIPYA: Wazee na wenye kinga dhaifu kupewa chanjo ya ziada Rwanda

Rwandani.png #KirusiKIPYA: Wazee na wenye magonjwa hatarishi waanza kupewa chanjo ya ziada Rwanda

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: BBC

Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza kuwa itaanza kutoa dozi ya tatu kwa wazee na wale ambao wana maradhi nyemelezi kuanzia leo Jumanne.

Wizara hiyo inasema utekelezaji huo utafanywa kwa awamu na utaanza katika mji mkuu, Kigali.

Waziri wa nchi wa Rwanda anayehusika na huduma za afya ya msingi anasema dozi ya tatu itatolewa kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 50.

Wale kati ya miaka 30 na 50 watapata tu chanjo ya ziada ikiwa wana maradhi nyemelezi .

Shirika la Afya Ulimwenguni linasema kikundi hiki kinapaswa kupata chanjo ya ziada, kwani wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa baada ya chanjo yao ya kwanza.

Wafanyakazi wa afya pia wanastahiki dozi ya tatu.

Kati ya idadi ya watu wapatao milioni 13, zaidi ya Wanyarwanda milioni tatu wamechanjwa hadi sasa.

Chanzo: BBC