Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kirusi kipya cha COVID-19 chagundulika Afrika Kusini

Ask Immune Cold Flu SuperJumbo V2 Kirusi kipya cha COVID-19 chagundulika Afrika Kusini

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: BBC

Watafiti wanachunguza aina mpya ya virusi vya corona nchini Afrika Kusini. Virusi hivyo aina ya C.1.2, ambavyo huzaana mara mbili zaidi lakini havijatajwa kuwa vyenye kutia wasiwasi.

Matukio ya virusi hivyo yamerekodiwa katika kila mkoa nchini Afrika Kusini pamoja na mataifa saba ya Afrika, bara Asia, Ulaya na maeneo ya Oceania.

Wanasayansi wanatathmini jinsi aina hiyo ya virusi inavyokabiliana na viini vinavyopigana na corona. Pia wanachunguza jinsi vinavyozaana na maambukizi yake.

Maria van Kerkhove, afisa wa kiufundi anayeongoza uchunguzi huo kwa niaba ya shirika la la Afya duniani WHO amesema kwamba virusi hivyo havionekani vikiongezeka.

Amesema kwamba aina hiyo ya virusi ndio inayoendelea kuwaathiri wengi na kwamba WHO itaufahamisha umma iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote.

Afrika kusini ni taifa ambalo limeathiriwa vibaya na aina zote mbili za maradhi ya corona ikiwemo yale ya virusi vya Delta na Beta ambayo yanasambazwa kwa urahisi zaidi.

Taifa hilo limesajili maambukizi 2,770,575 ya virusi vya corona ikiwemo vifo 81,830.

Chanzo: BBC