Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kirusi Kipya hatari kwa binadamu chagundulika Guinea

UGONJWA Kirusi cha Marburg

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa Afya nchini Guinea pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)wamethibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa ugonjwa huo hatari kuonekana Afrika Magharibi ambapo kesi ya kwanza iligundulika katika mkoa wa Kusini mwa Gueckedou.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Dk Matshidiso Moeti amesema kuwa kuna uwezekano wa virusi hivyo kuenea mbali na kwa ukubwa hivyo wanahitaji kuuzuia kwa kila namna haraka iwezekanavyo.

"Hii ni mara ya kwanza kwa ugonjwa huu unaoambukiza sana unaosababisha homa ya kutokwa na damu, kutambuliwa nchini, na Afrika Magharibi,"

Ugonjwa wa Marburg unaangukia kwenye kundi moja na virusi vinavyosababisha Ebola ambao ni ugonjwa mwingine mbaya na wa kuambukiza sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live