Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kirinyaga: Wanafunzi 15 wanaswa wakibugia pombe siku ya kufunguliwa kwa shule

0fgjhs736ib4fnuld Kirinyaga: Wanafunzi 15 wanaswa wakibugia pombe siku ya kufunguliwa kwa shule

Mon, 10 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Maafisa wa polisi mtaani Gichugu kaunti ya Kirinyaga wamewakamata wanafunzi 15 baada ya kunaswa wakiwa walevi kwenye nyumba moja ya kukodisha.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa eneo hilo Antony Mbogo amesema wanafunzi hao ni miongoni mwa wasichana waliopatikana kwenye nyumba hiyo katika soko ya Mucangara.

" Tumethibitisha kwamba wanafunzi hao wanatoka katika shule tofauti za sekondari na walitarajiwa kurejea shuleni hii leo Jumatatu, Mei 10 na wengine Jumanne Mei 11," Mbogo alisema.

Mbogo pia alisema maafisa wa polisi walinasa pombe aina ya Ice Vodka, tayari walikuwa wamekunywa zaidi ya chupa nne.

Polisi walisema watatumia chupa hizo kama ushahidi dhidi ya washukiwa watakapofikishwa mahakamani.

Aidha, polisi pia walipata kadi za kucheza kamara na mipira za kondomu ambazo zilikuwa zimetumika, ishara kwamba wanafunzi hao walishiriki tendo la ndoa.

Mbogo alisema wanafunzi hao sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kianyaga na watafikishwa katika mahakama ya Gichugu Jumatatu, Mei 10.

Haya yanajiri huku shule kote nchini zikitarajiwa kufunguliwa Jumatatu, Mei 10 baada ya likizo ya wiki saba.

Likizo hiyo ilikuwa refu kwa ajili ya kuruhusu wanafunzi wa darasa la nane na wa kidato cha nne kufanya mitihani yao ya kitaifa.

Tayari matokeo ya mithani hiyo yametolewa ambapo mwanafunzi bora zaidi kote nchini alijizolea alama ya 433.

Katika mtihani wa kitaifa wa KCSE, wanafunzi 893 waliweza kupata gredi ya A, mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka wa kwanza kwa alama 87.334.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke