Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipindupindu kinavyozitesa nchi za Kusini mwa Afrika

Sadc Yakataa Wito Wa Kutangaza Dharura Ya Afya Ya Kipindupindu Kipindupindu kinavyozitesa nchi za Kusini mwa Afrika

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlipuko mkali wa kipindupindu kwa sasa umesababisha kero kubwa jamii za nchi za Kusini mwa Afrika, katika kile ambacho wataalam wanasema ni janga mbaya zaidi kulikumba eneo hilo kwa zaidi muongo mmoja.

Maelfu ya watu wamekufa, na maelfu ya wengine wameambukizwa na ugonjwa huo wa kuhara katika angalau nchi saba. Katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi, milipuko hiyo ililazimisha mamilioni ya wanafunzi kusalia nyumbani mnamo Januari.

Katika eneo lote, vituo vya kukabiliana na dharura vimechipuka katika uwanja wa shule na viwanja vya michezo, na vimejaa wagonjwa wanaougua kwa maumivu. Hofu inaongezeka kwamba ikiwa milipuko hiyo haitashughulikiwa hivi karibuni, wafanyikazi wa afya wanaweza kuzidiwa.

Katika wito wa dharura wa kushughulikia mlipuko huo mapema mwezi huu, viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walisema wanajitahidi kukomesha kuenea, lakini ukosefu wa maji safi, ukaguzi dhaifu wa mipaka, na uhaba wa chanjo ulimwenguni ni mambo yanayoweza kuvuriga azma hiyo.

Tangu Januari 2022, takriban watu 188,000 wameambukizwa kipindupindu katika nchi saba za SADC ambazo ni Zambia, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Tanzania, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Zaidi ya watu 4,100 wamefariki dunia, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu, OCHA.

Ugonjwa huo umekuwa ukienea tangu mwaka wa 2022. Zambia iliripoti kisa chake cha kwanza Oktoba 2023 ambapo zaidi ya watu 18,804 waliambukizwa kufikia Alhamisi iliyopita, katika kile serikali inasema ni mlipuko mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Takriban watu 658 wamekufa tangu Oktoba.

Malawi, ikiwa na angalau kesi 59,000 tangu mapema 2022, pia inaripoti mlipuko wake mkubwa wa kipindupindu kuwahi kutokea. Nchini Zimbabwe, kesi 21,000 tangu Februari 2023 zinafanya janga hili kuwa la pili kuwahi kurekodiwa. DRC, ambayo pia ni mwanachama wa SADC, ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya watu 71,000, wakati Afrika Kusini imerekodi idadi ndogo ya kesi, kwa watu 1,076.

Kipindupindu huenea wakati watu wakunywa maji au kula chakula ambacho kimechafuliwa. Ugonjwa huu ni wa kawaida katika maeneo yenye hali duni ya usafi wa mazingira, au katika maeneo yenye migogoro ambapo vyanzo vya maji ya kunywa vinaweza kuambukizwa na kinyesi au maji machafu kutoka kwenye mifereji ya maji machafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live