Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipindupindu chaua wanajeshi 14 DRC

SADC Waingia DRC Kipindupindu chaua wanajeshi 14 DRC

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani wanajeshi 14 wamekufa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na wengine 500 wameathiriwa na mlipuko wa kipindupindu Kusini-Mashariki mwa Mkoa wa Haut-Katanga, jeshi limeeleza katika taarifa yao.

Jenerali Eddy Kapend, Kamanda wa eneo la 22 la kijeshi, kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Mura, alithibitisha vifo hivyo wakati wa mkutano na ujumbe kutoka ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) mjini Lubumbashi.

"Kufikia saa 72 zilizopita, idadi ya wagonjwa wanaopokea matibabu iliongezeka hadi 144. Tumerekodi vifo 14 na tumeokoa wagonjwa wengi ambao wamerejea katika viwango vyao,” Jenerali Kapend amesema na kuongeza kuwa mlipuko huo ulisababishwa na hali mbaya katika kambi ya kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live