Walioharamishwa wa Mungiki, Maina Njenga baada ya kunasa bunduki mbili na misokoto ya bangi katika nyumba inayohusishwa naye katika kaunti ya Nakuru magharibi.
Katika taarifa yake ya Jumatatu, Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI) - ilisema kuwa vitu hivyo vilipatikana kufuatia msako mkali wa wapelelezi katika kijiji cha Ngomongo wiki iliyopita.
Polisi walisema kuwa washukiwa wanane wa kundi la Mungiki walikamatwa wakati wa uvamizi huo.
Bw Njenga alikuwa ameitwa kufika katika makao makuu ya polisi mjini Nakuru mnamo Jumatatu, lakini alishindwa kufanya hivyo na badala yake akajificha, vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti.
Afisa wa upelelezi mjini Nakuru Kopro Eliud Misoi, alisema watu wanane waliokamatwa wanashukiwa kuwa wanachama wa genge la uhalifu lililopangwa.
Haya yanajiri wiki chache baada ya nyumba za Bw Njenga zilizopo katika mji mkuu Nairobi na kaunti ya Laikipia kuripotiwa kuvamiwa na maafisa wa usalama kwa sababu zisizojulikana.
Mungiki ni dhehebu la siri ambalo lilipigwa marufuku mwaka wa 2002 baada ya kushutumiwa kuhusika na vurugu.