Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa zamani wa Kenya ahimiza wanajeshi zaidi kupelekwa DR Congo

Kiongozi Wa Zamani Wa Kenya Ahimiza Wanajeshi Zaidi Kupelekwa DR Congo Kiongozi wa zamani wa Kenya ahimiza wanajeshi zaidi kupelekwa DR Congo

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamehimizwa kuharakisha uwekaji wa wanajeshi wa ziada katika kikosi cha kikanda kinachotumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, mpatanishi wa jumuiya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anasema wanajeshi zaidi wanatakiwa kuchukua nyadhifa katika maeneo ambayo makundi yenye silaha yamejiondoa, kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano ya Luanda.

Bw Kenyatta alionyesha wasiwasi wake kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika jimbo la Kivu Kaskazini ambako waasi wa M23 wamepambana na vikosi vya usalama katika wiki za hivi karibuni.

Uganda na Sudan Kusini zinapanga kutuma wanajeshi baada ya wanajeshi kutoka Burundi na Kenya kuwasili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka jana kusaidia kumaliza miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu.

Bw Kenyatta alikaribisha wito wa hivi majuzi wa kusitishwa kwa uhasama na pande zote katika mzozo huo na viongozi wa Afrika Mashariki.

Katika taarifa yake, mratibu huyo wa mazungumzo ya amani alisema ataimarisha mipango ya duru ya nne ya mazungumzo jijini Nairobi kwa kuhamasisha uungwaji mkono wa kikanda na kimataifa kwa mkutano huo.

Amezitaka pande zote zinazohusika kuharakisha utekelezaji wa maazimio ya mazungumzo ya tatu ya mashauriano jijini Nairobi.

Pia ameomba msaada wa haraka wa kibinadamu kwa zaidi ya watu nusu milioni waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Mzozo huo umezorotesha uhusiano na DR Congo, ambayo inaituhumu nchi jirani ya Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23.

Rwanda inakanusha tuhuma hizo.

Chanzo: Bbc