Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa waasi DR Congo ahukumiwa maisha jela

Mtanzanianews 127064235 134138588493468 4456196214734733265 N 660x400 Kiongozi wa waasi DR Congo ahukumiwa maisha jela

Tue, 24 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Aliyekuwa Kiongozi wa Wanamgambo katika taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ntabo Ntaberi amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo ubakaji wa watu wengi.

Mahakama ya kijeshi ilimkuta na hatia ya mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono na kuwasajili watoto walio chini ya miaka 15 katika jeshi lake.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo iliochukua takriban miaka miwili ambapo waathiriwa 178 walitoa ushahidi wao.

Umoja wa Mataifa(UN) unasema kwamba umauzi huo umeonesha ‘uzoefu wa kutenda uhalifu bila kujali una kikomo chake’.

‘Uamuzi huo unawapatia matumaini waathiriwa wa mzozo huo wa DRC, mateso waliopitia yamesikilizwa na kutambuliwa’, amesema Leila Zerrougui, mkuu wa ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa uliopo nchini DR Congo.

WALIOIBA KOFIA YA POLISI, VIATU WABURUTWA KORTINI “WALIMKATA NA KISU”

Chanzo: millardayo.com