Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, kurejea kwenye mgomo wa kula

Senegal Upinzani Kula Tena Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, kurejea kwenye mgomo wa kula

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, ambaye anashikiliwa korokoroni tangu mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, kwa mashtaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi, amesema kwamba ameamua kurejea kwenye mgomo wake wa kula ambao alikuwa ameusimamisha mwanzoni mwa Septemba.

Sonko, 49, ambaye alikuwa mgombea wa uchaguzi wa urais wa mwezi Februari 2024 huko Senegal na ambaye katika uchaguzi wa rais wa 2019 aliibuka mshindi wa tatu, anamshtumu Rais Macky Sall, kwamba anafanya njama za kumzuia asishirikia tena kwenye uchaguzi.

Rais Sall, aliyechaguliwa mwaka wa 2012 kuongoza Senegal kwa kipindi cha miaka saba na akachaguliwa tena mwaka wa 2019 kwa ajili ya kipindi cha miaka mitano, alitangaza mapema mwezi Julai kwamba hatagombea tena urais. Rais Macky Sall wa Senegal

Katika sehemu moja ya matamshi yake, Ousmane Sonko amesema kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na X kwamba: "Tunaweza tu kutumia njia za upinzani ambazo hali yetu ya sasa inaruhusu. Ndiyo maana nimeamua kurudisha mgomo wangu wa kula.”

Lengo la kiongozi huyo wa kambi ya upinzani aliyeko korokoroni huko Senegal ni kuonesha "mshikamano" wake na wanaharakati wengine kwa "kukamatwa isivyo haki kutokana tu kutoa maoni yao ya kisiasa", kuwekwa kizuizini, na kunyimwa "mawasiliano yoyote na wapendwa wao."

Siku ya Ijumaa, Sonko alipandishwa tena kizimbani na jaji aliamuru arejeshwe kwenye orodha ya wapiga kura baada ya kuondolewa. Hukumu hiyo ya mahakama imefungua ukurasa mpya dhidi ya Serikali ya Macky Sall.

Hukumu hiyo itamruhusu Sonko, aliyeko kizuizini tangu mwishoni mwa mwezi Julai kuwa na matumaini ya kushiriki katika uchaguzi wa rais.

Mwishoni mwa Julai, Sonko alihukumiwa kufungwa kwa mashtaka mengine, ikiwa ni pamoja na kuitisha uasi, kushiriki katika wa uhalifu na kuhatarisha usalama wa serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live