Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani auawa, mwili wakutwa na risasi kibao!

Cherubin Okende Kiongozi wa upinzani auawa, mwili wakutwa na risasi kibao!

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Cherubin Okende ameuawa kwa kupigwa risasi huku mwili wake ukikutwa ukiwa umejaa risasi katika Mji Mkuu wa Kinshasa.

Okende ambaye ni mwanachama wa Chama cha upinzani cha Together for the Republic alikutwa amefariki kwenye gari lake siku ya Alhamisi asubuhi kwa mujibu wa kiongozi wa chama, Mbazi Kasongo.

Mwili wa Okende ambaye amewahi kuwa waziri wa Uchukuzi umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti huku mazingira ya kifo chake yakiwa bado hayajafahamika.

Mauaji ya Okende yanakuja huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya chama tawala cha Rais Felix Tshisekedi na wapinzani wake wa kisiasa kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Disemba huku wanachama kadhaa wa upinzani wakitiwa mbaroni wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.

Okende alikuwa mmoja wa mawaziri kadhaa waliojiuzulu kutoka chama tawala na alikuwa msemaji wa kiongozi mkuu wa upinzani na Rais wa Chama cha Together for Republic, Moise Katumbi.

Katika ujumbe wake kwenye ukurasa wa Twitter, Katumbi ambaye ana uwezekano wa kuwa mgombea wa Urais kupitia Chama hicho alisema kuwa mwenzake aliuawa na kutaka uchunguzi huru ufanyike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live