Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani Senegal atishia kuvuruga uchaguzi

Kiongozi Wa Upinzani Senegal Kiongozi wa upinzani Senegal atishia kuvuruga uchaguzi

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Voa

Kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko, hana mpango wa kutafuta maridhiano, na Rais Macky Sall, na ameashiria kuwa anaweza kujaribu kuvuruga uchaguzi wa mwaka ujao, ikiwa hataruhusiwa kugombea, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha France 24 siku ya Alhamisi.

"Hakutakuwa na uchaguzi katika nchi hii, iwapo Rais Macky Sall atapinga kugombea kwangu," Sonko alisema kutoka nyumbani kwake katika mji mkuu wa Dakar, ambako amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani, tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka miwili, mwezi Juni, kwa mashtaka yaliyotokana na madai ya ubakaji.

Sonko amekanusha mashtaka hayo na kusema kuwa yanalenga kumzuia kushiriki katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Februari, mwakani.

Sonko, maarufu miongoni mwa vijana wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, aliitisha maandamano kufuatia hukumu hiyo ya mwezi Juni.

Ghasia zilianza, ambapo maelfu ya waandamanaji walichoma majengo na magari, na kuwarushia mawe maafisa wa polisi, ambao walijibu kwa kurusha mabomu ya machozi na, baadhi ya mashahidi wanasema, risasi za moto.

Takriban watu kumi na sita walipoteza maisha yao.

Machafuko hayo yalichochewa, kwa kiasi kikubwa, na wasiwasi kwamba Sall angewania muhula wa tatu madarakani, katika uchaguzi wa mwezi Februari. Sall, tangu wakati huo amesema hatagombea.

Chanzo: Voa