Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani Senegal aondolewa katika orodha ya wagombea urais

Sonko Kitabuni Kura Kiongozi wa upinzani Senegal aondolewa katika orodha ya wagombea urais

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Katiba la Senegal Jumamosi lilichapisha orodha ya mwisho ya wagombea 20 wa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo Februari 25 ambayo haiwajumuishi kiongozi wa upinzani aliyefungwa Ousmane Sonko, na Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade.

Walioorodheshwa katika orodha hiyo ya wagombea wa kiti cha urais ni pamoja na Waziri Mkuu Amadou Ba, aliyeteuliwa na Rais Macky Sall kama mrithi wake baada Sall kutangaza mnamo Julai kwamba hatawania muhula wa tatu.

Rais Macky Sall wa Senegal Wengine waliotajwa katika orodha hiyo na Baraza la Katiba la Senegal ni Mawaziri Wakuu wa zamani na mahasimu Idrissa Seck na Mahammed Boun Abdallah Dionne, Meya wa zamani wa mji wa Dakar Khalifa Sal na Bassirou Diomaye Diakhar Faye ametajwa kama mgombea mbadala wa Sonko. Faye mwenye umri wa miaka 43 mwanachama wa chama cha Sonko kilichovunjwa pia yuko kizuizini lakini bado hajashtakiwa.

Sonko, ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa Rais wa 2019 nchini Senegal amekuwa katika mzozo mkubwa na serikali ambao umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live