Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani Rwanda afanya mgomo wa kula mahabusu

Kayumba Rwanda Christopher Kayumba, Kiongozi wa upinzani Rwanda

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, Christopher Kayumba amefanya mgomo wa kula baada ya kukamatwa na polisi, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha ubakaji.

Kiongozi huyo kutoka chama cha siasa cha Rwandese Platform of Democracy,alikamatwa tarehe 09, Septemba mwaka 2021 kwa tuhuma hizo za ubakaji.

Taarifa iliyotolewa na mwanasheria wake inaeleza kuwa kiongozi huyo amegoma kula ikiwa ni katika kupinga mashtaka hayo ambayo kwa mujibu wa Jeshi la Polisi ni kuwa alifanya vitendo hivyo kati ya 2012 na 2017kuwa madai hayo ni ya uchochezi wa kisiasa.

Awali kabla ya kukamatwa kwake, kiongozi huyo ambaye pia ni muhadhiri wa chuo Kikuu aliwahi kuitwa na Jeshi hilo mwezi Marchi mwaka 2021 na kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

Na siku mbili kabla ya kukamatwa kwake, Rais Kagame alitoa witokwa Jeshi la Polisi nchini humo kuhakikisha linachukua hatua kali juu ya wahalifu wa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live