Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa upinzani DRC atangaza kujiunga na waasi wa M23

M23 Upinzani DRC.jpeg Kiongozi wa upinzani DRC atangaza kujiunga na waasi wa M23

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anayeishi uhamishoni Corneille Nangaa ametangaza kuunda Kitengo cha Kisiasa cha Kijeshi kitakachokuwa mshirika wa kundi la Waasi wa M23 na makundi mengine yenye silaha ili 'kuiokoa nchi'

Hali kisiasa na usalama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekuwa na wasi wasi mkubwa kuelekea uchaguzi wa Desemba 20 mwaka huu

Nangaa ambaye ni Mkuu wa zamani wa Tume ya Uchaguzi ametoa tangazo hilo akiwa Nairobi Jijini Nairobi, nchini Kenya ambapo kwenye kufikisha ujumbe huo alikuwa sambamba na Bertrand Bisimwa “rais” wa kundi la M23 kwenye Hoteli moja katika mji mkuu wa Kenya

Vitendo vyao vimesababisha zaidi ya watu milioni moja kukimbia nyumba zao ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa Hali ya wasi wasi imeongezeka zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa wiki ijayo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live