Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa serikali ya Niger atangaza baraza la mawaziri la mpito

Kiongozi Wa Serikali Ya Niger Atangaza Baraza La Mawaziri La Mpito Kiongozi wa serikali ya Niger atangaza baraza la mawaziri la mpito

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa serikali ya Niger Jenerali Abdourahmane Tchiani ameteua baraza la mawaziri kinyume na wito wa viongozi wa eneo hilo wa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Baraza la mawaziri lilitangazwa kwenye TV ya serikali saa sita saba unusu kwa saa za eneo siku ya Alhamisi.

Serikali mpya inaundwa na mawaziri 21, wakiwemo manaibu waziri na mjumbe wa waziri.

Serikali mpya ya mpito, inayoundwa na wanajeshi na raia, inaongozwa na Waziri Mkuu wa muda Lamine Zeine Ali Mahamane, ambaye pia atahudumu kama waziri wa uchumi na fedha.

Aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi Lt Jenerali Salifou Mody, anayechukuliwa kama naibu wa Jenerali Tchiani, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi wa taifa.

Kanali Maj Abdourahmane Amadou, ambaye amekuwa akisoma taarifa nyingi kwenye TV ya serikali tangu mapinduzi ya Julai 26, ni waziri wa vijana na michezo.

Tayari jeshi hilo limewataja wakuu wapya wa kijeshi na kuwafuta kazi maafisa wengi wakuu wa serikali waliohudumu katika utawala wa Bw Bazoum.

Chanzo: Bbc
Related Articles: