Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa serikali ya Gabon akataa kuchukua mshahara wa rais

Kiongozi Wa Serikali Ya Gabon Akataa Kuchukua Mshahara Wa Rais Kiongozi wa serikali ya Gabon akataa kuchukua mshahara wa rais

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema amesema anaachana na mshahara wake kama rais na atapokea tu mshahara kama kamanda wa walinzi wa jamhuri.

Amekua rais wa muda kufuatia kupinduliwa kwa Rais Ali Bongo mwezi Agosti.

Tangazo la Jumatano usiku lilitolewa na msemaji wa serikali ya kijeshi, ambaye alisema Jenerali Nguema alichukua uamuzi huo kwa sababu "anafahamu dharura za kijamii na matarajio mengi ya watu wa Gabon".

"Kila siku inayopita inaruhusu [junta] kufahamu zaidi hali ya jumla ya kuzorota kwa nchi na hasa fedha za umma," Kanali Ulrich Manfoumbi alisema.

Utawala wa miaka 14 wa Rais aliyeondolewa madarakani Bongo ulikumbwa na madai ya ufisadi na kashfa nyingine za kifedha, huku serikali ikisema kuwa fedha za nchi hiyo ni "mhanga wa ghadhabu halisi ya uhalifu".

Mbali na kukataa mshahara wake akiwa rais, Jenerali Nguema pia aliamua kupunguza matumizi ya fedha za umma kwa kuwakata posho wabunge, kuondoa fedha za kisiasa na kukata posho za vikao.

Rais alisema hii itaongeza mapato ya serikali.Hatua ya hivi punde imeonekana kama jaribio la kurejesha imani ya watu wa Gabon katika uongozi wa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live