Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa mpito wa Mali azungumza na Rais wa Urusi

Kiongozi Wa Mpito Wa Mali Azungumza Na Rais Wa Urusi Kiongozi wa mpito wa Mali azungumza na Rais wa Urusi

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goïta alizungumza kwa simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin ambapo walitoa wito wa suluhu ya kisiasa nchini Niger, ambapo mapinduzi ya Julai yalimwondoa madarakani Rais Mohammed Bazoum.

Kikosi tawala nchini Niger kilikuwa kimeonya dhidi ya uingiliaji kati wa kigeni wenye lengo la kumrejesha madarakani Bw Bazoum baada ya kambi ya kiuchumi ya kanda ya Afrika Magharibi Ecowas kusema kuwa jeshi ni chaguo la kubadilisha mapinduzi hayo.

Wanajeshi wa Mali walikuwa wameapa kuwaunga mkono wenzao nchini Niger endapo watakuwa na uvamizi kutoka nje na wameendeleza uhusiano wa karibu na Urusi na mamluki wa Wagner wanaoungwa mkono na Kremlin.

Bw Putin pia alimpa pole Kanali Goïta kutokana na shambulizi la kigaidi lililotokea kaskazini-mashariki mwa Mali wiki jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

"Marais walizungumza kwa kiasi kikubwa kuhusu hatua za kivitendo kwa ajili ya maendeleo zaidi ya ushirikiano kati ya Urusi na Mali katika maeneo mbalimbali, kama vile biashara, uchumi na nyanja za kibinadamu, pamoja na juhudi za kukabiliana na ugaidi," taarifa ya Kremlin ilisema.

Bw Goïta pia alimshukuru Bw Putin kwa kuunga mkono nchi yake wakati wa kura ya hivi karibuni ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuondoa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Mali.

Mapema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Urusi ilipiga kura ya turufu azimio la kurejesha vikwazo kwa Mali ili kuongeza muda wa kundi la wataalamu wanaohusika na ufuatiliaji wa dhuluma zinazofanywa na makundi yenye silaha na vikosi vya usalama vya Mali.

Chanzo: Bbc