Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa mapinduzi Niger: Niko tayari kumwachia huru Bazoum

Niger Kiongoziii.jpeg Kiongozi wa mapinduzi Niger: Niko tayari kumwachia huru Bazoum

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

iongozi wa mapinduzi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, amekutana na ujumbe wa wanazuoni wa Kiislamu wa Nigeria, huku mashinikizo za kikanda na kimataifa yakiongezeka dhidi ya utawala wa kijeshi wa Niamey kwa shabaha ya kurejesha utawala wa kikatiba.

Duru za habari zinasema, Tiani amesisitiza katika mazungumzo ya pande hizo mbili kwamba hapingi suala la kuachiliwa huru rais aliyezuiliwa, Muhammad Bazoum, lakini amekataa kurejea kwake madarakani.

Ujumbe wa wanazuoni wa Kiislamu wa Nigeria unaoongozwa na Abdullahi Bala Lau, uliwasili mjini Niamey Jumatano wiki hii na kukutana na Jenerali Abdourahamane Tiani katika ziara yake ya pili tangu baada ya mapinduzi hayo.

Awali baraza la kijeshi linalotawala Niger lilikaribisha upatanishi wa ujumbe wa wanazuoni wa Kiislamu wa Nigeria kwa shabaha ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Niger.

Katika muktadha wa juhudi zinazohusiana na utatuzi wa mgogoro Niger, Abdulsalami Abubakar, rais wa zamani wa Nigeria na mkuu wa ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) katika mazungumzo na baraza la kijeshi la Niger, amesema mkuu wa baraza la kijeshi la nchi hiyo, Jenerali Abdourahamane Tiani, amekataa ombi la ujumbe huo la kumrejesha madarakani Rais Muhammad Bazoum.

Vinara wa mapinduzi ya kijeshi, Niger Mkuu wa ujumbe wa ECOWAS ameongeza kwamba, Tiani amesema kuwa, kuachiliwa Bazoum kunawezekana iwapo makubaliano yatafikiwa, lakini hatarejeshwa madarakani.

Tiani pia amesisitiza katika mazungumzo hayo kuwa muda wa kipindi cha mpito ni miaka 3, na ametoa wito wa kufunguliwa mipaka iliyofungwa na kurejeshwa umeme nchini Niger kutoka nchi jirani ya Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live