Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, anazuru taifa la Djibouti, kwa ziara inayoonekana kutafuta ungwaji mkono dhidi ya wapiganaji wa RSF ambao wamekuwa kwenye vita wanajeshi wake tangu April mwaka huu.
Ni zaira inayojiri wakati huu vita vikiendelea nchini Sudana kati ya wapiganaji war sf na jeshi la serikali, ziara inayolenga kujikita katika swala la usalama kati ya latafa hayo mawili na kanda nzima, kwa mjibu wa msemaji wa baraza la uongozi wa Sudan, Mohammed al-Sammani.
Ziara hiyo pia inalenga kutathimini nafasi ya Sudan katika maswala ya amani na usalama barani Afrika, hasa kutoka na mchango wa mataifa ya kikanda katika kutafuta siluhu kwa mzozo wa mataifa mengine ya pembe ya Afrika.
Licha ya Sudan kutaka muungano wa mataifa ya IGAD kusuluhisha mzozo unaoendelea nchini humo, nchi hiyo imesisitiza haja ya IGAD kutoingilia maswala ya ndani ya mataifa husika hasa hali ya kisiasa ya Sudan.
Al Burhana amefanya kikao na mwenyeji wake rais Ismail Omar.