Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa kijeshi Mali afanya mazungumzo na Putin

Putin Mali Kiongozi wa kijeshi Mali afanya mazungumzo na Putin

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa mpito wa Mali Kanali Assimi Goïta amesema kuwa alifanya mazungumzo ya simu siku ya Jumatano na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Katika chapisho kwenye Twitter, Bw Goïta alisema: ‘’Tulizungumza kuhusu Shirikisho la Urusi kuunga mkono serikali ya mpito kisiasa, na nilisifu ubora wa ushirikiano wetu, ambao unaheshimu uhuru wa Mali na matarajio ya watu wake.’’

Siku ya Jumanne, jeshi la wanahewa la Mali lilizindua rasmi ndege kadhaa mpya za kivita zilizotolewa na Urusi wakati wa hafla iliyoongozwa na Bw Goïta katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bamako.

Ndege za kivita za enzi ya Usovieti ni kundi la hivi punde zaidi la usafirishaji wa kijeshi kutoka Moscow chini ya uhusiano wa karibu kati ya Urusi na Mali tangu jimbo la Sahel lilipokumbwa na mapinduzi Agosti 2020.

Mali imeegemea Urusi baada ya kutofautiana na nchi za Magharibi, hususan Ufaransa, ambayo inapinga uwepo wa mamluki wa Wagner katika nchi ya Sahel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live