Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa kanisa lenye utata Kenya akamatwa

POLISI KENYA Kiongozi wa kanisa lenye utata Kenya akamatwa

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: Voa

Mhubiri mwenye utata nchini Kenya anayehusishwa na vifo vya watu 4 waliofariki kwa njaa kufuatia mafundisho ya kidini yenye misimamo mikali amekamatwa.

Polisi nchini Kenya wanaamini kuwa Makenzie Nthenge ndiye anayehusika na dhehebu la kidini katika eneo la Kilifi katika pwani ya Kenya, ambapo wafuasi wake walikuwa tayari kufunga hadi kufa baada ya kushawishika kuwa ilikuwa njia ya mkato ya kukutana na Yesu.

Watu 11 waliokuwa wagonjwa mahututi wanaohusishwa na kanisa hilo lenye utata la Good News International wanapata ahueni hospitalini baada ya kuokolewa kutoka mafichoni eneo la kijijini.

Wengine walikuwa wameripotiwa kufunga kwa muda wa siku 21 bila chakula.

Bw Nthenge alisema alikuwa amefunga majengo ya kanisa lake mwaka wa 2019, lakini yeye pia ni mwinjilisti na anaendesha chaneli ya you tube, ambayo inaonekana kuwavutia wafuasi kutoka mamia ya maili.

Mwezi uliopita tu Bw Nthenge alishtakiwa kuhusiana na vifo vya watoto wawili ambao wazazi wao walikuwa wamejiunga na kanisa hilo, na wanaaminika kufuata mafundisho yake.

Chanzo: Voa