Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa jeshi Sudan asema yupo tayari kuzungumza na kamanda wa waasi

Kiongozi Wa Jeshi Sudan Asema Yupo Tayari Kuzungumza Na Kamanda Wa Waasi Kiongozi wa jeshi Sudan asema yupo tayari kuzungumza na kamanda wa waasi

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa jeshi Sudan aiambia BBC kuwa yupo tayari kuzungumza na kamanda wa vikosi vya waasi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anasema yupo tayari kimsingi kuzungumza na Mohamed Hamdan Dagalo, kiongozi wa Rapid Support Forces (RSF).

Wawili hao wamekuwa wakipambana vita vikali vya ndani tangu Aprili, ambavyo Umoja wa mataifaunasema umesababisha vifo vya zaidi ya watu 5000 na wengine zaidi ya milioni 5 wameachwa bila ya makaazi.

Jenerali Burhan, aliyedhibiti uongozi kupitia mapinduzi mnamo 2021, alikuwa akizungumza na BBC katika mahojiano baada ya kuhotubia mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa mjini New York.

Analiongoza jeshi la Sudan SAF na anafanya ziara ya kidiplomasia kimataifaakitafuta uungwaji mkonolicha ya kushindwa kukabidhi uongozi kwa utawala wa kiraia.

Kiongozi huyo wa jeshi amekana kuwa kikosi chake kinawalenga raia, licha ya Umoja wa mataifa na mashirika ya misaada kusema kwamba kuna Ushahidi kuwa wanarusha makombora ya anga ayanayolenga makazi ya watu.

Burhan anasema ana imani atapata ushindi, lakini amekiri kwamba amelzamika kuhamisha makao yake makuu hadi Port Sudan kwasababu vita katika mji mkuu Khartoum vimefanya kuwa vigumu kwa serikali kuendelea na shughuli.

Kadhalika amesema atakaa chini na Jenerali Dagalo – anayefahamika kama Hemedti ili mradi atimize ahadi ya kuwalinda raia iliotolewa na pande zote katika mazungumzo yaliofanyika Jeddah, Saudi Arabia, mnamo Mei.

Katika ujumbe wa video wiki hii Hemedti amedai kuwa yuko tayari kwa mazungumzo ya kisiasa. Viongozi wote wamezungumza kuhusu kusitisha mapigano katika siku za nyuma, lakini mpaka sasahilo halijasaidia kupungua kwa mapigano .

Jenerali Burhan amekana kwamba Sudan itaishia kuwa na utawala ulioshindwa kama Somalia au nchi iliogawanyika kama Libya.

Umoja wa mataifa unasema hakuna upande unaoonekana kukaribia kupata ushindi wa kijeshi.

Chanzo: Bbc