Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa dhehebu tata nchini Kenya aachiliwa na kukamatwa tena

Kiongozi Wa Dhehebu Tata Nchini Kenya Aachiliwa Na Kukamatwa Tena Kiongozi wa dhehebu tata nchini Kenya aachiliwa na kukamatwa tena

Tue, 2 May 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa dhehebu tata la Kenya na wengine sita wamekamatwa tena dakika chache baada ya mahakama ya Malindi kuwaachilia huru.

Hakimu Ivy Wasike aliwaachilia huru Paul Nthenge Mackenzie na washirika wake baada ya maombi ya upande wa mashtaka kufunga faili hiyo.

Mwendesha mashtaka wa serikali Vivian Kambaga alisema alitaka wahukumiwe katika mahakama nyingine - kwa mashtaka ambayo yatajumuisha ugaidi.

Wamekamatwa nakusafirishwa hadi kaunti jirani ya Mombasa.

Hapo awali walishtakiwa kwa mdhehebu hilo la kidini kupatikana kwenye makaburi ya pamoja mwezi uliopita.

Bw Mackenzie, kiongozi wa dhehebu hilo, alishtakiwa kwa kuwahimiza wajiue kwa njaa. Amepinga kuhusika na kosa lolote.

Ripoti ya uchunguzi wa maiti ilionyesha kuwa baadhi ya wahasiriwa pia waliuawa kwa kukosa hewa na kunyongwa

Chanzo: Bbc