Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa Upinzani akamatwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kiongozi Wa Upinzani Akamatwa Nchini Jamhuri Ya Afrika Ya Kati Kiongozi wa Upinzani akamatwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imethibitisha kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Crépin Mboli Goumba huko Bangui.

Waziri wa Haki Arnaud Djoubaye Abazene aliambia BBC kuwa Bw. Mboli-Goumba anazuiliwa kutokana na madai aliyotoa dhidi ya mahakama.

Kiongozi huyo wa upinzani anayeongoza Kambi ya Republican ya Kutetea Katiba (BRDC) ni mkosoaji mkubwa wa serikali.

Inasemekana alihutubia mkutano wa waandishi wa habari siku chache zilizopita ambapo alishutumu "mafia wa mahakama", wanaohusishwa na mzozo wa mali isiyohamishika ambao unamgombanisha na familia ya rais wa zamani André Kolingba.

Pia alikuwa amemshutumu Waziri wa Sheria, Arnaud Djoubaye Abazène kwa kuingilia kati.

Lakini Waziri alisema kukamatwa huko kunahusishwa na malalamiko ya kudharau mahakama ya kikundi cha mahakimu na mawakili, ambayo yaliwasilishwa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuomba kufunguliwa mashitaka kwa Bw Mboli-Goumba.

Chama cha upinzani cha Republican Bloc for the Defense of the Constitution kimekosoa "kukamatwa kiholela" kwa kiongozi wake.

Taarifa ya Martin Ziguelé, msemaji wa chama hicho ilieleza kuwa Bw. Mboli-Goumba alitaka kuondoka nchini kwa "sababu za kiafya" alipokamatwa katika uwanja wa ndege wa Bangui M'Poko.

"Tumepokea kwa masikitiko na uchungu taarifa za kukamatwa kna kuzuiliwa kwa mratibu wa BRDC Maitre Crépin Mboli Goumba, Jumapili Machi 3, 2024, mjini Bangui,'' ilisema taarifa hiyo.

Chama hicho kinataka kiongozi huyo aachiwe huru mara moja.

Serikali haijasema ni lini inatarajia kumfungulia mashtaka mahakamani.

Lakini wakosoaji wanaamini inaweza kuwa jaribio la kukandamiza sauti muhimu nchini humo

Chanzo: Bbc