Kikosi cha wanamgambo nchini Sudan kimechapisha video ya kiongozi wake kwenye mtandao wa Twitter akiwahutubia wapiganaji - kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo kuzuka mwezi Aprili.
Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama "Hemedti", alionekana mwembamba kwenye video hiyo na wachambuzi wanasema mkono wake mmoja unaonekana kana kwamba hauko sawa.
Kumekuwa na uvumi kuwa kamanda huyo ambaye ana umri wa miaka 40 hivi amejeruhiwa katika vita hivyo.
Hotuba yake ilijumuisha matamshi yake ya mara kwa mara dhidi ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi ambaye anakabiliana naye katika mzozo mkali wa utawala wa nchi hiyo.
Alisema iwapo uongozi wa jeshi hilo utabadilika, atakubali makubaliano ya amani ndani ya saa 72.
Hemedti aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kupitia safu ya wanamgambo wa Janjaweed, wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kikabila wakati wa mzozo wa Darfur.
RSF iliundwa na Rais wa zamani Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani kufuatia maandamano ya umma mwaka 2019.
Kiongozi wa RSF aliunga mkono kuondolewa kwake kama njia ya kujiingiza katika nafasi yenye nguvu zaidi.
Lakini muungano wake na Jenerali Burhan ulisambaratika vibaya miezi mitatu iliyopita. Tangu vita kuanza RSF imehamia katika maeneo mengi ya makazi ya miji mitatu inayounda Khartoum Kubwa - Bahri, Khartoum na Omdurman - ambayo mara nyingi hukumbwa na mashambulizi ya anga. Katika hotuba yake,
Hemedti alikuwa na tabia mbaya sana kuhusu Yasir al-Atta, afisa wa ngazi ya juu wa jeshi ambaye anaongoza operesheni huko Omdurman.
Aliomba msamaha kwa watu wa Sudan kwa "maafa ya vita", ambayo alishikilia kuwa yamewekwa kwa RSF.
Akiwa amezungukwa na wapiganaji wenye silaha katika kanda hiyo ya video ya dakika tano, pia alikanusha kuwa wale wanaotuhumiwa kwa uporaji mkubwa mjini Khartoum na kwingineko walikuwa wanachama wa RSF.