Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa M23 arejera DRC kuongoza mashambulizi

M23 Sultan.png Kiongozi wa M23 arejera DRC kuongoza mashambulizi

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda mkuu wa kundi la waasi la M23 Generali Sultani Makenga amerudi mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, akitokea nchi Jirani ambayo msemaji wa kundi hilo Maj. Willy Ngoma hakutaja.

Maj. Ngoma amesema kwamba tangu arudi DRC, Generali Sultani Makenga amekuwa akitembelea wapiganaji wake katika sehemu mbali mbali mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo katika mji wa Bunagana ambao sasa unadhibitiwa na waasi wa M23.

Makenga, mwenye umri wa miaka 50, anasemekana kujua vizuri nguvu na uwezo wa jeshi la DRC, na eneo zima la kivu kaskazini.

Wachambuzi wanasema kwamba lengo la Makenga ni kutoa maelezo Zaidi kwa wapiganaji wake namna ya kupambana na jeshi la DRC na wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki endapo wataingia Congo.

“Bila shaka Generali Sultani Makenga amerudi DRC kutoka kule amekuwa amejificha, ili kuongoza mashambulizi mwenyewe. Amekuwa akiongoza akiwa mbali na sasa yupo na makamanda wake na wapiganaji. Hii ni kuwapa motisha kuendelea kupigana Zaidi.” Amesema Nabende Wamoto mchambuzi wa siasa za maziwa makuu akiwa Kampala, Uganda, katika mahojiano kwenye kipindi cha radio cha kwa undani (saa tatu hadi saa tatu na nusu usiku, Afrika mashariki), idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, VOA.

M23 Wanadhibithi Bunagana, waliwahi kudhibithi Goma Waasi wa M23 waliwahi kudhibithi mji wa Goma mnamo mwaka 2012 lakini wakalazimika kuondoka kutokana na shinkizo la aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Barack Obama.

Mkubwa wa General Makenga wakati huo, Generali Bosco Ntaganda, aliyejulikana kama Terminator, na ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa - ICC, alikuwa amekataa kuamuru wapiganaji wake kuondoka Goma kabla ya aliyekuwa rais wa DRC wakati huo Joseph Kabila, kukubali matakwa ya waasi wa M23.

Makenga, alikataa kumsikiliza Ntaganda na akaamurisha wapiganaji wa M23 kuondoka Goma, hatua ambayo ilimkasirisha Ntaganda.

Uhasama kati ya Generali Sultan Makenga na General Bosco Ntaganda ulipelekea mpasuko katika kundi hilo na kutokea mapigano makali kati ya wapiganaji watiifu kwa kila upande, yaliyopelekea vifo vya wapiganaji kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live