Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi wa Ghana adai fidia ya utumwa kwa mataifa ya Afrika

Kiongozi Wa Ghana Adai Fidia Ya Utumwa Kwa Mataifa Ya Afrika Kiongozi wa Ghana adai fidia ya utumwa kwa mataifa ya Afrika

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Ghana Akufo-Addo ametaka malipo ya fidia kwa mataifa ya Afrika kutokana na dhuluma za kihistoria za biashara ya utumwa iliyovuka Atlantiki.

Akizungumza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano, alisisitiza kuwa huu ndio wakati wa kuweka mada ya ulipaji fidia mbele. Alisema dunia kwa karne nyingi haikuwa tayari na haiwezi kukabiliana na matokeo ya biashara ya utumwa.

Alisema "fidia lazima zilipwe" , akiongeza kuwa ingawa hakuna fedha zinazoweza kufidia hali ya kutisha ya biashara ya utumwa, ingeleta hoja kwamba mamilioni ya Waafrika "waliozalisha" waliwekwa kazini bila kulipwa fidia.

Si mara ya kwanza kwa rais wa Ghana kuzungumza kuhusu fidia, mwaka jana alisema muda ulikuwa umechelewa ili kuongeza mijadala kuhusu suala hilo.

Kisha akatoa wito wa kuomba radhi rasmi kwa mataifa ya Ulaya ambayo yalihusika katika biashara hiyo, na kuutaka Umoja wa Afrika kuwashirikisha diaspora ili kuendeleza kazi ya fidia.

Biashara ya watumwa iliyovuka Atlantiki, ambayo iliathiri mamilioni ya Waafrika, ilikuwa uhamiaji mkubwa zaidi wa kulazimishwa katika historia na moja ya unyanyasaji wa kibinadamu, kulingana na UN.

Kuhama kwa Waafrika kulienea katika maeneo mengi ya ulimwengu kwa kipindi cha miaka 400. Ghana ilikuwa mojawapo ya vituo vya kuondoka kwa wengi wa wale waliokuwa watumwa huko Afrika Magharibi.

Chanzo: Bbc