Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi mwandamizi wa Sudan adhuru Ethiopia

Dagalo.crdownload Dagalo anafahamika kuongoza kikosi katili nchini mwake

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi mwandamizi wa Sudan Mohamed Hamdan Dagalo anakwenda Ethiopia leo, kwa ziara ya nadra ya afisa wa serikali ya Khartoum tangu mataifa hayo mawili yalipotumbukia kwenye mivutano kuhusu mipaka.

Shirika la habari la Sudan SUNA limeripoti kuwa Dagalo, ambaye ni kiongozi wa pili wa ngazi ya juu katika Baraza la Tawala la kijeshi nchini Sudan, atakuwa Ethiopia kwa siku mbili ili kukutana na maafisa kadhaa wa nchi hiyo.

Afisa huyo wa Sudan ni mkuu wa kikosi maalumu chenye nguvu cha RDF, kinachoogopwa kutokana na rikodi yake ya vitendo vya ukatili hasa katika jimbo la magharibi la Darfur. Mahusiano kati ya Sudan na Ethiopia yamezorota kutokana na mzozo juu ya eneo la mpaka linalozozaniwa la Al-Fashaqa Magharibi ambalo kila upande linadai haki ya umiliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live