Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi mwandamizi Tigray akimbia Ethiopia

Ethtrg.png Kiongozi mwandamizi Tigray akimbia Ethiopia

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban mwaka mmoja tangu mapigano yalipoanza katika Jimbo la Tigray nchini Ethiopia, kiongozi wa Serikali ya mpito jimboni humo ameikimbia nchi akihofia usalama wake.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa mnadhimu wa jimbo hilo, Gebremeskel Kassa ameliambia Shirika la Habari AFP kwamba usalama wake upo shakani hivyo anatafuta hifadhi nje ya Ethiopia.

Kassa aliingia madarakani muda mfupi baada ya vikosi vya jeshi vinavyoongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kupambana na wafuasi wa chama tawala jimboni humo cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) tangu Novemba mwaka jana.

Abiy alisema uamuzi wa kuviruhusu vikosi vya jeshi kupambana na raia hao ulisukumwa na matukio yao ya TPLF kilichoiongoza Ethiopia kwa miongo mitatu mpaka mwaka 2018, kuvamia baadhi ya kambi za jeshi.

Mwezi kama huu mwaka jana, Kassa alikuwa mstari wa mbele kupinga mashambulio yaliyokuwa yanafanywa na majeshi ya Eritrea yaliyokuwa yanashirikiana na askari wa Ethiopia akivitaka vikosi hivyo viondoke jimboni humo.

Vilevile, alivituhumu vikosi vya askari walioingia kutoka jimbo jirani la Amhara kwamba vimechangia kuwatawanya wananchi wa Tigray waliolazimika kuyahama makazi yao.

Kassa alitoroka nchini mwake mwishoni mwa Juni baada ya wapiganaji waaminifu TPLF waliyachukua tena baadhi ya maeneo muhimu jimboni Tigray yakiwamo makao makuu ya Mekele.

Katika taarifa yake ya kuomba hifadhi iliyoonwa na AFP, Kassa amesema aliitwa kwenye mkutano na maofisa waandamizi walioalumu Serikali ya mpito kwa udhaifu wa jeshi.

“Tuhuma hazina ushahidi wowote wa haki kwa sababu tunaendesha Serikali ya kiraia,” anasema Kassa kwenye maombi hayo ambaye aliiomba AFP kutotaja nchi anayoomba hifadhi hiyo kwa sababu za kiusalama zaidi.

Taarifa za kuomba hifadhi nje ya Ethiopia zimekuja siku chache baada ya vikosi vya ulinzi na usalama jijini Addis Ababa kumshikilia Abraha Desta, ofisa mwingine mwandamizi katika Serikali ya mpito ya Tigray ambayo hivi karibuni meitisha mkutano wa majadiliano ya mgogoro uliopo katika ya Serikali Kuu na ile ya jimbo.

Kassa ameiambia AFP kwamba maofisa wa Serikali Kuu nchini Ethiopia kwa muda mrefu walikuwa wanakataa kufanya mazungumzo ya kuumaliza mgogoro uliopo kuanzia Desemba iliyopita baada ya vikosi vya TPLF kuondolewa kweny emiji ya Tigray.

“Walikataa. Walisema ‘jeshi la TPLF limevunjwa lote sasa kama hali ni hiyo tutazungumza na nani?’” alikumbuka.

Kassa alisema kadri vikosi vya majeshi ya Ethiopia yalivyokuwa yanawashambulia waasi wa Tigray katika Mkoa wa Amhara, angani na ardhini, yalikuwa ni mashambulizi yaliyovuka mipaka.

Mpaka sasa mamia ya maelfu ya watu wa Tigray wanakabiliwa na majanga yanayotokana na ukame jambo ambalo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Kassa anaiomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kati ili kuwanusuru wananchi wanaoteseka ndani ya nchi yao.

“Iwapo jeshi hili (la Ethiopia) likiweza kujipenyeza mpaka ndani kabisa ya Tigray, hiyo itakuwa dhahama na huo utakuwa muda wa jumuiya ya kimataifa kujuta,” alisema Kassa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live