Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiongozi kundi la waasi Msumbiji auawa na vikosi vya kijeshi

Mozambiq Picdead Kiongozi kundi la waasi Msumbiji auawa

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa kikundi cha waasi cha Renamo kutoka chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji ameuawa na jeshi la nchini humo.

Vikosi vya ulinzi na Usalama nchini humo FDS, vimetangaza kuwa Mariano Nhongo, Mkuu wa kikundi hicho mwenye msimamo mkali wa upinzani katika taifa hilo kuwa ameuwawa katika mashambulizi na jeshi hilo.

FDS, imesema kuwa kiongozi huyo aliuawa pamoja na wapambe wake katika jimbo la Sofala majira ya saa moja asubuhi mara baada ya mashambulizi makali yaliyofanyika katika moja ya msitu aliokuwa akiutumia kujificha jimboni humo.

Inaelezwa kuwa kundi hio limepigana vita ya zaidi ya miaka 16 na chama tawala cha Frelimo kabla ya kuingia madarakani mwaka 1992 na hapo ndio kilipokuwa chama kikuu cha upinzani hadi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live